music 4rever

Videos

Friday, 5 October 2018

USHAHIDI: Bora mniuwe, Tupac hajafa yupo Malaysi

Mtoto wa rapper nguli nchini Marekani, Suge Knight ajulikanaye kwa jina la Suge J. Knight ametoa ushahidi kuwa Tupac Shakur hajafa bado yupo hai, na stori zote zinazoandikwa kuwa alikufa ni za uongo kwani yupo nchini Malaysia  na mwenye afya njema.


Suge J. Knight ameweka ushahidi huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonesha baadhi ya picha na meseji za Tupac, huku akimtaka 50 Cent naye aongee ukweli kuhusu kufichwa kwa Tupac.
Knight alianza kutoa ushahidi kupitia ukurasa wake wa Instgram, ambapo aliweka posti ya kwanza iliyokuwa na maneno yaiyosomeka  “Tupac is alive.” akimaanisha Tupac ni mzima.




Baada ya posti, aliombwa na wafuasi wake aoneshe ushahidi na yeye akaamua kuweka posti nyingine iliyokuwa na Meseji (iMessage) akionywa na watu aliowaita Illuminati wakimtaka aachane na taarifa hizo la sivyo watampoteza.
“Unaongea sana, huu ni muda wako kuondoka” naye akawajibu “Ukweli utajulikana na siendi popote pale”.






Akaamua kuweka kabisa ushahidi wa picha na video za Tupac, huku akieleza kuwa ni picha za sasa hivi za Tupac akiwa nchini Malaysia , “Wanawadanganya nyie tu, huyu jamaa yupo hai”.



Hata hivyo, ameshambuliwa na baadhi ya watu wakimwambia kuwa anawatoa watu kwenye reli baada ya baba yake wiki hii kuhukumiwa kifungo cha miaka 28 jela kwa kosa la kugonga mtu na gari na kukimbia.
Baba yake, Suge Knight ambaye kwa sasa yupo jela, inatajwa kuwa alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye mipango hiyo ya kifo cha Tupac.
Mnamo September 7, 1996, Shakur alipigwa risasi kadhaa akiwa barabarani huko Las Vegas, Nevada. Alikuwa akitoka kwenye pambano la ngumi kati ya Mike Tyson na Bruce Sheldon.
Mpaka sasa mamilioni ya watu ulimwenguni wanaamini kuwa Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi, lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja juu ya kifo hicho.
Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 30 walidaiwa kulipwa kusaidia kudanganya kifo hicho wakiwemo polisi, madaktari na mashuhuda na mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kuongea.


BOFYA HAPA TAZAMA VIDIO ALIVYOKUWA AKIONGEA TUPAC
Share:

Related Posts:

0 maoni:

Post a Comment

Gallery

Featured Posts

Column Right

Search This Blog

Carousel

Feat

Definition List

Recent Posts